Kuzuia udanganyifu

Pamoja na kuongezeka kwa ulaghai wa kidigitali na majaribo ya hadaa, ni muhimu kujua jinsi ya kuepuka kuwa mwathirika. Tunahimiza watumiaji wote kujua jinsi ya kutambua na kuepuka hadaa.

Ishara za utapeli wa hadaa

Makosa ya uandishi

Majaribio mengi ya uthibitishaji yana makosa ya maandishi na sarufi, kwani matapeli kawaida hawaweki maudhui kupitia waandishi wataalamu.

Viunganishi vya mashaka na viambatisho

Ujumbe wa hadaa una viunganishi vyenye madhara na viambatisho vya kutoa data yako ya kibinafsi au kusakinisha programu hasidi. Viunganishi hivi vina makosa ya maandishi ya tovuti halisi au vimehifadhiwa kwenye vikoa vya mashaka na visivyo salama.

Uharaka

Kujenga hisia ya haraka, hofu, au msisimko kukudanganya na kukufanya uchukue maamuzi ya haraka ni mbinu ya kawaida ya utapeli. Wanataka ukurupuke, kwa hivyo utoe maelezo yako na ukamilishe muamala haraka bila kufikiria.


Ahadi za kupata pesa kwa urahisi

Tapeli atadai umeshinda pesa na kuomba nenosiri au nambari ya benki yako. Deriv kamwe haiombi taarifa zako binafsi au za kifedha kupitia mitandao ya kijamii, wala hatutoi zawadi/promosheni. 


Watumaji wasiojulikani

Majaribio ya hadaa hutoka kwa anwani za barua pepe na wasifu wa mitandao ya kijamii sawa na zetu lakini zina makosa ya kiuandishi katika majina yao. Weka imani tu kwenye taarifa zilizochapishwa kutoka kwenye wasifu za mitandao ya kijamii zilizoorodheshwa chini ya tovuti yetu.


Mbinu bora za kuepuka ulaghai

Usibonyeze viunganishi haraka

Weka kishale chako juu ya URL kabla ya kubonyeza ili uone kiunganishi. Ikiwa kiunganishi hakilingani na kikoa chetu au kinaonekana kuwa na shaka, usikibonyeze.

Usipakue faili

Usifungue viambatisho na vipanuzi kama .exe, .com, .bat, na.scr., lakini unaweza kufungua kama ulikuwa unavitarajia. Aina hizi za faili zinaweza kuwa na programu hasidi.

Usichukue hatua mara moja

Usifanye malipo au kutoa taarifa binafsi ikiwa unahimizwa kufanya hivyo. Tutakufikia kupitia barua pepe zinazoishia @deriv.com, info.deriv.com, au kupitia mazungumzo mubashara ikiwa inahitajika.

Usitoe taarifa binafsi

Usitoe taarifa binafsi bila kuthibitisha mtumaji. Mambo yote ya siri yanafanywa kupitia WhatsApp au gumzo ya moja kwa moja na timu yetu ya Msaada kwa Wateja.

Usijibu jumbe

Zuia simu zisizojulikana, ripoti barua pepe zenye shaka, na wasiliana na timu yetu ya Msaada kwa Wateja ikiwa utakutana na wasifu wenye shaka kwenye mitandao ya kijamii.

Usiogope kuuliza

Wasiliana nasi kupitia mazungumzo mubashara ikiwa hauna uhakika juu ya barua pepe au wasifu wa mitandao ya kijamii, na tutathibitisha ikiwa ni kutoka Deriv. 


Rasilimali za hadaa Deriv

Kama sehemu ya juhudi zetu endelevu za kukuza jamii salama ya biashara mtandaoni, 
tembelea viunganishi vifuatavyo ili kuchunguza zaidi juu ya: