75% ya akaunti za wawekezaji wa rejareja hupoteza pesa wanapofanya biashara ya CFDs na Deriv. Unapaswa kuzingatia ikiwa unaweza kumudu kuchukua hatari kubwa ya kupoteza pesa zako.

CFD ni vyombo tata vyenye hatari kubwa ya kupoteza pesa haraka kutokana na leverage. 75% ya akaunti za wawekezaji wa rejareja hupoteza pesa wanapofanya biashara ya CFDs na mtoa huduma huyu. Unapaswa kuzingatia ikiwa unaelewa jinsi bidhaa hizi zinavyofanya kazi na ikiwa unaweza kumudu kuchukua hatari kubwa ya kupoteza pesa zako.

Ninawezaje kuwatambua matapeli wanaojifanya ni watu wa msaada kwa wateja toka Deriv kwenye Telegram?

__wf_reserved_inherit
Mfano wa vikundi vinavyoiga Deriv kwenye Telegram

Lengo kuu la tapeli ni kuiba taarifa zako muhimu na fedha zako.

Hizi ni baadhi ya njia za kutambua wajifanyao kuwa huduma kwa wateja wa Deriv:
- Wajifanyao wanauliza maelezo yako ya kuingia au taarifa nyingine nyeti kupitia Telegram.
- Wanatoa zawadi zinazoonekana kuwa nzuri mno hivi kwamba haziwezi kuwa za kweli.
- Wanadai malipo kupitia njia zisizoweza kufuatiliwa, kwa mfano, kupitia cryptocurrency.
- Wanakwambia upakue app ambayo haijatolewa kwenye Google Play Store au Apple App Store.
- Wanakwambia upakue programu inayoruhusu kifaa chako kudhibitiwa kwa mbali.
- Wanakwambia upakue faili zenye programu hasidi au virusi vinavyoweza kuathiri kifaa chako.

Bila shaka, orodha hii haijakamilika. Kila siku, matapeli wanakuja na mbinu mpya kujaribu kuiba taarifa zako na pesa.